JARIDA WAKILI MKUU/ Toleo Na. 10
Abstract
Toleo la Kumi la Jarida la Wakili Mkuu ni maalumu kwa ajili ya kuendelea kuangazia mafanikio ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) katika miaka mitatu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kuangazia hilo, Jarida hili linaendelea kutambua mchango mkubwa wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maeneo ya bajeti, ujenzi wa Ofisi kwenye mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma, usimamizi wa mashauri, mifumo ya usimamizi wa mashauri na
udhibiti ubora, mafunzo kwa watumishi wa OWMS,ushirikiano wa Ofisi na wadau, maboresho ya mifumo ya TEHAMA ambayo kwa kiasi kikubwa yameboresha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ndani na nje ya nchi.