JARIDA WAKILI MKUU/ Toleo Na. 9
Abstract
Ninayo furaha kubwa kuungana tena na wasomaji wetu wapendwa kwenye Toleo la Tisa la Jarida la Wakili Mkuu. Jarida hili ni Maalumu kwa ajili ya kuangazia majukumu yaliyotekelezwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) kwa kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Disemba, 2023 ikihusisha uendeshaji wa mashauri mbalimbali yenye maslahi mapana kwa Taifa kama vile uhalali wa uwepo wa Pori laAkiba la Paloleti Wilayani Ngorongoro, ujenzi wa bomba la mafuta na uwekezaji katika Bandari ya Dar es salaam