JARIDA LA WAKILI MKUU: TOLEO LA SABA
Abstract
Toleo la Saba la Jarida la Wakili Mkuu wa Serikali ni maalumu kwa ajili ya kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kutimiza miaka mitano tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018. Katika kipindi cha miaka mitano, Ofisi inatambua mchango mkubwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katka kuboresha Ofisi hii ili kuiwezesha kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhakikisha inaiwakilisha vyema na kwa weledi mkubwa katika uratibu, usimamizi na uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi yaliyofunguliwa na au dhidi ya Serikali na taasisi zake ndani na nje ya nchi. Aidha, napenda kuishukuru menejimenti na watumishi wote wa Ofisi hii chini ya uongozi wa Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Nalija Luhende kwa mchango wao mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hii kwa kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.